Raisi wa Uganda Yoweri Museven alipokuwa katika mazungumzo na raisi wa DR Congo Jeseph Kabila
Na
Martha Saranga AminiMazungumzo ya amani kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kundi la waasi la M 23 lililoshindwa na jeshi la serikali huenda yakarejelewa tena jijini Kampala.
Hatua hiyo inajiri baada ya rais Joseph Kabila kukutana na rais Yoweri Museveni alipositisha kwa muda ziara yake mashariki mwa nchi DRC na kuelekea mjini Kampala Uganda kwa mazungumzo na raisi wa taifa hilo Yoweri Kaguta Museveni kuhusu hatma ya mazungumzo ya Kampala baada ya kusambaratishwa kwa kundi la waasi wa M23.
Mwezi mmoja uliopita vikosi vya serikali ya DRC kwa kusaidiwa na vile vikosi maalum vya Umoja wa Mataifa vilivyoko mashariki mwa nchi hiyo walifanikiwa kuwafurusha waasi wa kundi la M23 waliokuwa wakikalia maeneo mengi ya mashariki ya nchi hiyo.
Kabla ya kuondoka mjini Goma raisi Kabila aliwaomba raia wa eneo hilo kuwa na subira na serikali yake inajipanga upya kuanza utekelezaji wa miradi ya maendeleo baada ya kulishinda kundi la M23.
Katika hatua nyingine ndege zisizokuwa na rubani zinaanza kutumika leo jumanne huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo ili kusaidia kuimarisha usalama katika mpaka Kwa mara ya kwanza ndege hizo zisizokuwa na rubani kutoka Italia ndizo zinaanza kufanya uchunguzi na kuimarisha hali ya utulivu katika eneo la Mashariki mwa DRC.
Hatua ya Umoja wa Mataifa imelenga kufuatilia harakati za makundi ya uasii katika maeneo ya Kivu, wakati huu kukiwa na taarifa kuhusu raia kukimbia makazi wakielekea katika mpaka wa DRC na Rwanda.
www.hakileo.blogspot.com