Shujaa Mandela alitetea haki za Palestina


Vyombo vya habari vya Magharibi vimepuuza msimamo wa shujaa Nelson Mandela wa kutetea haki za Wapalestina.
Ingawa hayati Mandela amepewa umuhimu mkubwa na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi lakini nukta moja ya misimamo yake imepuuzwa, nayo ni upinzani wake mkali wa sera za ubaguzi za utawala haramu wa Israel. Mandela ambaye aliaga dunia Desemba 5 akiwa na umri wa miaka 95 alikuwa muungaji mkono mkubwa wa harakati za kupigania ukombozi za Palestina. Shujaa Mandela alilinganisha mapambano ya ukombozi wa Palestina na mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.

Ikumbukwe kuwa katika kilele cha kampeni zake dhidi ya ubaguzi wa rangi, Mandela alilaaniwa na nchi nyingi za Magharibi zikiongozwa na Marekani. Alituhumiwa kuwa ni gaidi na hata alibakia katika orodha ya magaidi ya Marekani hadi mwaka 2008. Harakati za Mandela za kupinga ubaguzi wa rangi zimekuwa ilhamu kwa Wapalestina wanaopigana dhidi ya ubeberu na ukatili wa Israel.

Harakati ya Kiislamu ya Kupigania Ukombozi Palestina Hamas imemtaja Mandela kuwa 'mwanamapambano mkubwa.' Msemaji wa Hamas Mussa Abu Marzuq amesema, 'Mandela alikuwa mmoja kati ya waungaji mkono wakubwa zaidi wa harakati za kupigania ukombozi Palestina.'
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company