UCHAMBUZI WA HABARI: ZUMA ANAPOZOMEWA, NA THABO MBEKI PIA..!



Ndugu zangu,

Kwenye shughuli ya jana ya kumuaga Mzee Madiba kule Afrika Kusini, kulisikia sauti za kumzomea Rais Jacob Zuma, na Thabo Mbeki pia alizomewa.

Naam, Afrika hatuzomeani misibani. Na isitoshe Rais wa Nchi hazomewi. Na kama inatokea, basi, kuna jambo, na si dogo hata kidogo!

Tafsiri yake?

Majuzi hapa niliandika yafuatayo kuhusu Mandela na Uongozi. Mandela alipata kutamka;

" The leader must keep the forces together, but you can't do that unless you allow dissent. People should be able to criticise the leader without fear of favour. Only in that case are you likely to keep your colleagues together"- Nelson Mandela. It is when Mandela gave a piece of advice to newly elected Party Leader, Thabo Mbeki at the ANC Congress in Mafikeng, 1997.

Naam, ilikuwa ni mwaka 1997. Mzee Mandela alikuwa akitoa ushauri kwa Thabo Mbeki, mrithi wake.

Na jana nikamsikiliza msomi akichambua hali ya mambo kwenye televisheni ya BBC, ni William Gumede, ni mwandishi wa kitabu hicho pichani. Bahati nzuri ninacho kwenye maktaba yangu. Na ndiko nilikoikuta kauli hiyo ya Mandela hapo juu.

Alichokiona na kukisema mwandishi William Gumede jana usiku kwa kiasi kikubwa nakubaliana nacho. Kwamba baada ya Mandela kuondoka, na huku kukiwa na Uchaguzi Mkuu mwakani, basi, ANC itapita kwenye mtihani mgumu.(P.T)


Mandela alikuwa ndiye nguvu ya kuunganisha, na mengine yalikuwa yanamezewa kwa vile Madiba yupo. Maana , vijana kumzomea Rais wa nchi msibani si jambo jema, lakini, si jambo la kupuuzia. Tumesikia sauti za wenye kusema ni jambo dogo hilo, la kupuuziwa.

Naam, kwenye siasa muhimu ni kuangalia alama za nyakati. Maana, Thabo Mbeki halikuwa chaguo la Mzee Mandela. Cyril Ramaphosa ndio lilikuwa chaguo la Mandela, lakini, wakati ulimtaka Mandela amweke kando Ramaphosa na badala yake kumchagua Thabo Mbeki.

Na jana wakati vijana wakimzomea Zuma uwanjani tukamsikia Makamu wa Rais wa ANC, Cyril Ramaphosa akitamka;
" Please, I am asking for your discipline".

Naam, baada ya Mzee Madiba kuondoka kwenye ' Kijiji Cha ANC' bila shaka, ANC, kabla na baada ya uchaguzi wa mwakani, itahitaji kuwa na uongozi imara, utakao- keep forces together, and not by not allowing dissent.
Good morning!
Maggid Mjengwa.
Iringa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company