Mikhaïlo Koval, atuliwa kuwa waziri wa Ulinzi wa Ukraine


Waziri mpya wa ulinzi wa Ukraine, Mikhaïlo Koval.
REUTERS/Alex Kuzmin,Na RFI
Rais wa mpito wa Ukraine, Oleksandre Tourtchinov, amependekekeza bungeni jina la Mikhaïlo Koval ili kuchukua na fasi ya waziri wa ulinzi iliyokua ikishikiliwa na Igor Tenioukh, ambaye amejiuzulu mapema leo asubuhi. Waziri huyu mpya wa ulinzi ni afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la kulinda mipaka la Crimea, na aliwahi kushikiliwa kwa masaa kadhaa na kikosi kinachounga mkono Urusi.

Igor Tenioukh, ambaye amejiuzulu kwenye wadhifa huo, amekua akilaumiwa kwamba hakuwajibika vilivyo katika mgogoro wa Crimea.
Igor Tenioukh, amekua akinyooshewa kidole cha lawama kwamba amechangia kwa kile kinachoelezwa kujitenga kwa kisiwa cha Crimea na Ukraine, baada ya kuonekana kuwa hakutoa amri kwa jeshi ili likabiliane na hali ya mambo iliyokua ikijiri katika eneo hilo, wakati alikua amepewa uwezo wote na silaha za kutosha.

Kiongozi wa chama cha Udar, ambaye ni mwanamisumbi wa zamani,Vitali Klistchko ni mmoja mwa waliyotoa lawama zao dhidi ya waziri huyo aliyejiuzulu. Vitali Klistchko, ametishia kumuomba rais wa mpito wa Ukraine Oleksandre Tourtchinov ajiuzulu.

Amebaini kwamba kwa sasa afisa huyo anaeshikiliya kwa sasa wizara ya ulinzi ana kibarua kigumu cha ktoa ulinzi wa kutosha kwa taifa. Kauli hiyo inakuja wakati, serikali ya Ukraine ikifahamisha kwamba Urusi imekua ikiongeza idadi ya wanajeshi kwenye mpaka wake wa mashariki.

Jenerali Kovol, waziri mpya wa ulinzi, alizaliwa mwaka wa 1956, na aliteuliwa kuongoza kikosi cha wanajeshi wa kulinda mipaka katika kisiwa cha Crimea.

Machi 5, alishikiliwa kwa muda wa masaa kadhaa na kikosi cha wanajeshi waliyokua wanaunga mkono Urusi, ambao walidhibiti baadae kisiwa hicho kilipojitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company