E WAJUA MCHAKATO WA MAJI HUWATENGANISHA SAMAKI?



Mwani wa baharini (juu) na minyoo ya baharini (chini) ni mfano wa conformers



Na Josephine Thomas

Kwa nini baadhi ya samaki na viumbe wengine wanaweza kuishi katika maji ya bahari tu na wengine katika maji safi tu, si kinyume chake?

Hii ni rahisi ! Ni kutokana na mchakato wa kuhama kwa maji unaojulikana kama Osmosisi . Huu ni mchakato wa maji kuhama kutoka sehemu moja yenye kiwango cha chini cha chumvi kwenda sehemu yenye kiwango cha juu cha chumvi.

Pia ni uwezo wa maji kuingia au kutoka ndani na nje ya seli hai ya viumbe , katika kukabiliana na mkusanyiko wa kiwango cha chumvi mpaka usawa kufikiwa.

Viumbe baharini hujibu hali hii kwa kuwa katika hali ya aidha kutokuikabili osmosisi (osmotic conformers) au kuikabili osmosisi (osmotic regulator).

Wasioweza kuikabili osmosisi

Viumbe vya baharini wasioweza kuikabili osmosisi, miili yao haiwezi kupingana na mchakato wa osmosisi ya asili. Seli zao zina kiwango cha chumvi sawa na mazingira wanayoishi. Wao ni pamoja na mimea ya bahari na wanyama wenye uti wa mgongo ambao hawawezi kuishi vizuri katika maeneo bila ya kiwango cha kawaida cha chumvi ya baharini ipatayo 35 (sehemu kwa maelfu) .

Ikitokea hawa viumbe hawa conformers wamewekwa katika maji safi (yasiyo na chumvi ), osmosisi itasababisha maji safi kuingia katika seli yao (kutoka katika kiwango kidogo cha chumvi kwenda kiwango kikubwa) na hatimaye kusababisha seli zao kupasuka.
Kama wakiwekwa katika maji yenye chumvi zaidi ya ile ya baharini zaidi ya 35, basi itasababisha maji ndani ya seli kutoka na kuhamia nje , hatimaye seli pukuchuliwa na kusinyaa kwa kukosa maji.



Samaki aitwaye 'Arctic charr' (juu) na Nyangumi (chini) ni mfano wa viumbe wanaoikabili osmosisi.




Wanaoweza kuikabili osmosisi

Viumbe hawa huwa na aina ya utaratibu wa udhibiti wa osmosisi na chumvi ndani ya miili yao kiasili. Kwao haijalishi kiwango cha chumvi maudhui ya maji baharini ana sehemu waliyopo, wao huweza kuzuia mabadiliko yoyote katika seli hai zao. Viumbe hawa ni pamoja na samaki, nyoka, ndege na mamalia.

Mfano bora wa kundi hili ni samaki ajulikanaye kama salmon. Samaki huyu ana kiwango cha chumvi kipatacho 18 (chini ya kiwango cha chumvi cha maji ya bahari amabayo ni 35). Endapo samaki huyu atawekwa katika maji ya bahari, maji yatatoka kutoka katika seli za mwili wake, lakini yeye atakabiliana na hali hii kwa kunywa maji ya bahari daima ili kuzuia seli kusinyaa. Wakati samaki huyu anahamia katika maji safi, basi yeye ataacha kunywa maji na figo yake kufanya kazi kuanza kuzalisha kiasi kikubwa cha mkojo ili kuondoa kiwango cha maji mwilini.

Makala kwa msaada wa Mhadhiri wa Chuo kikuu Huria cha Tanzania (OUT)

Bi Isabella Thomas - Dodoma
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company