Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya
Shindano la Tanzania Movie Talents Kwa kanda ya Nyanda ya Juu Kusini, Mkoani Mbeya limefikia Tamati kwa washindi watatu kutoka kanda hii ya nyanda ya juu Kusini Kupatikana na Kutangazwa na Majaji watatu.
Shindano hili kwa kanda ya nyanda Ya juu kusini limehitimishwa rasmi leo kwa washindi watatu kupatikana na hatimaye shindano hili litahamia Kanda ya Kusini na Usaili utafanyika Mkoani Mtwara
Shindano hili limelenga kuinua na kukuza vipaji vya kuigiza Tanzania na hatimaye kuendeleza vipaji hivi vya kuigiza Tanzania.
Usaili wa Shindano hili ni bure kabisa na fomu hupatikana eneo la usaili.