Shule ya wasichana waliotekwa nyara Nigeria
Maafisa wa usalama, wawindaji na walinzi wanaendelea kuwatafuta karibu wasichana 100 wa shule waliotekwa nyara kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wasichana hao walitekwa nyara na kundi la Boko Haram siku ya Jumatatu.
Jeshi limekana taarifa yake ya awali iliyosema kuwa wengi wa wasichana hao walikuwa wamefanikiwa kutoroka.
Karibu wasichana thelathini wameaminika kutoroka kutoka kwa watekaji wao lakini huenda wengine tisisini na tisa wakawa bado wanazuiliwa na wapiganaji hao.
Wengi wa wazazi wa wasichana hao pamoja na jamaa wengine, waliwasaka wasichana hao Ijumaa kutwa katika msitu hatari wa Sambisa.
Mmoja wa wazazi wa wasichana hao, alisema msitu huo sio mahala salama pa kulala na hivyo walilazimika kuondoka.
Aliambia BBC kuwa aliona mahala ambapo panaonekana kama kambi ya wapiganaji wa Boko Haram ambao hawaishi tena msituni humo.
Kulikuwa na magari pamoja na pikipiki na kisima cha maji lakini watu waliokutana nao msituni walisema kuwa hawana habari kuhusu wasichana waliotekwa nyara.
Haijulikani idadi kamili ya wasichana waliotekwa nyara. Maafisa wanasema 99 hawajulikani waliko lakini wazazi wanasema kati ya wasichana 150 na 200 bado hawajapatikana