Lee Joon-Seok nahodaha wa meli iliyozama ameomba radhi kwa yaliyotokea
Viongozi wa mashitaka nchini Korea Kusini wameiomba mahakama kutoa kibali cha kukamatwa kwa nahodha wa feri ya abiria iliyozama siku ya Jumatano ikiwa imewabeba zaidi ya watu 400.
Hadi kufikia sasa watu mia mbili na sabini hawajulikani waliko.
Jitihada za kutafuta karibu abiria mia mbili hamsini waliokuwa kwenye feri hiyo zinazidi kukumbwa na changamoto.
Juhudi za uokozi zingali zinaendelea kuwatafuta manusa wa ajali ya meli
Wapiga mbizi wanaojaribu kuingia ndani ya chombo hicho walifanikiwa kuingia eneo la mizigo lakini wakashindwa kuyafikia maeneo mengine
Mmoja wa wapiga mbizi hao alisema kuwa hawakufanikiwa kuiona vizuri feri hiyo hali iliyowalazimu kuiguza kwa mikono yao.
Afisa wa ulinzi wa pwani Ko Myung Suk amesema kuwa hawakupata manusura yeyote eneo walilofanikiwa kufika
Naibu mwalimu mkuu kwenye shule ambapo wengi wa wanafunzi walikuwa wakisomea amepatikana ameaga dunia.
Vyombo vya habari vinasema kuwa huenda mwalimu huyo amejitoa uhai.