ARSENAL wamefanikiwa kujihakikishia nafasi ya kucheza michuano ya UEFA kwa mwaka wa 17 mfululizo baada ya Everton kuchapwa mabao 3-2 na Manchester City na kumhakikishia Aserne Wenger kumaliza ligi si chini ya nafasi ya nne katika msimamo.
Mabao mawili ya Edin Dzeko na lingine kutoka kwa Sergio Aguero yametosha kumpatia ushindi Manuel Pellegrini na kupanda kileleni kwa ligi kuu.
Man City sasa hatima yao ya kubeba ubingwa imebaki katika mechi zao mbili za mwisho dhidi ya Aston Villa na West Ham ili kuchukua ubingwa wao wa pili wa ligi kuu katika misimu mitatu.
Asernal walitabiriwa kuchuana na Man City kutafuta ubingwa msimu huu na waliongoza ligi kwa muda mrefu kabla ya kuanza kupoteza mechi nyingi na kuwaacha Chelsea na Liverpool wakishindana na Manchester City mpaka sasa.
Kufungwa na Everton katika uwanja wa Goodison Park mwezi uliopita kulitaka kutia doa rekodi ya kushiriki UEFA kwa miaka 17 mfululizo, huku Roberto Martinez kwa upande wake toka siku hiyo amefungwa na Southampton, Crustal Palace na Manchester City.
Sasa Asernal wanajiandaa na michezo yao miwili ya mwisho dhidi ya West Bromwich Albion na Nowrich ili kujihakikishia nafasi yao ya nne na kuhamishia akili zao katika fainali ya FA.
Washaki bunduki hao wa London watakabiliana na Hull City kwenye uwanja wa Wembley mei 17 mwaka huu, huku wakiwa na matumaini ya kufuta ukame wa kutobeba makombe kwa miaka tisa sasa.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago