GERARDO Martino amesema yeye ndiye anatakiwa kulaumiwa kutokana na msimu mbaya wa Barcelona baada ya kulazimisha sare ya mabao 2-2 nyumbani Camp Nou dhidi ya Getafe katika mchezo wa La Liga.
Lionel Messi alikuwa wa kwanza kufunga bao la kuongoza dakika ya 23 kabla ya Angel Lafita kusawazisha dakika ya 42, lakini Alex Sanchez aliandika bao la pili dakika ya 67.
Barca wakiwa na matumaini ya kushinda mechi hiyo, dakika ya 90 ya mchezo, Lafita alizima ndoto zao baada ya kusawazisha bao la pili na matokeo kubakia 2-2, lakini Wakalunya hao bado wana matumaini ya kubeba ubingwa.
Martino baada ya mechi alisema: “Tulifanya makosa yaliyotugharimu. Timu ilikuwa na hamu ya kushidna”.
“Tulicheza vizuri na kustahili kushinda. Kiukweli sio msimu mzuri kwetu. Si kwangu tu hata klabu pia. Umekuwa msimu mgumo mno”.
“Nadhani anayewajibika kwa hili ni kocha anayeongoza timu. Kimahesabu, tumefanya kila jitihada kushinda taji.”.
“Tulihitaji kufanya vitu vingi zaidi, lakini hatutakiwa kukata tamaa mpaka siku ya mwisho”.
Martino aliendelea kwa kusema kumekuwa na matatizo klabuni ambayo yanatakiwa kutatuliwa, huku akionesha kutokuwa na wasiwasi juu ya hatima yake.
“Wachezaji wanajua nini kinaigawa timu na lipi chaguo sahihi”. Alisema.
“Bado kuna muda wa kueleza hatima yangu. Huwa sioni shida kuwajibika na nadhani nastahili kubeba lawama. Msimu huu kumekuwa na mapungufu yanayotakiwa kutatuliwa”
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago