FIFA WAPIGA CHINI OMBI LA FERNANDO KUTAKA KUICHEZEA URENO KOMBE LA DUNIA

SHIRIKISHO la soka duniani FIFA, limetupilia mbali maombi ya kiungo wa Porto, Mbrazil, Fernando kutaka kuichezea timu ya taifa ya Ureno katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil kuanzia juni 12 hadi julai 13.
Kiungo huyo mzaliwa wa Brazil alipata uraia wa Ureno mwezi desemba 2013, lakini anatakiwa kuiwakilisha Brazil katika mashindano ya kimataifa na si Ureno.
Baada ya Ureno kuona FIFA wamemruhusu Mbrazil, Diego Costa kuichezea Hispnia katika fainali za kombe la dunia mwaka huu, waliona ipo haja na wao kumuombea Fernando, lakini FIFA wameweka wazi kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 26 hawezi kuicheza Ureno.
FIFA wamesema Fernando anaweza kuicheze nchi yake aliyozaliwa kwasababu mwaka 2007 aliiwakilisha Brazil katika kampeni za kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 20.
Taarifa iliyotolewa na chama cha soka nchini Ureno jana inasema: “Chama cha soka nchini Ureno kimepokea taarifa leo hii (jana) kutoka FIFA kuwa mchezaji Fernando hawezi kuiwakilisha timu ya taifa ya Ureno”.
“FIFA wamesema mchezaji huyu hakuwa na uraia wa Ureno alipokuwa anaichezea Brazil kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 20 kama inavyotakakiwa na shirikisho”.
Fernando ambaye amecheza mechi 38 katika mashindano yote msimu huu akiwa na Porto, kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kujiunga na Machester City inayoshiriki ligi kuu soka nchini England.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company