KITENDO cha Manchester United kukosa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kutaipa hasara timu hiyo ya Pauni Milioni 30, imeelezwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward.
Pamoja na hayo, Woodward amesema kwamba haitaiathiri k;abu hiyo katika solo la usajili. "Kutokana na mikataba ya Televisheni, tunakadiria tutakosa Pauni Milioni 30 za michuano ya Ulaya. Matarajio ya klabu yalikuwa ni kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa naa utaona kwenye usajili wetu,".
Hasara: Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward (katikati) amesema klabu itakosa Pauni Milioni 30 kwa kutoshiriki michuano ya Ulaya
Mazungumzo: Giwji wa United, Ryan Giggs alipigwa picha nchini Uholanzi akiwa na kikao na Van Gaal Jumatano
Akizungumza katika mkutano wa simu, alisema: "Katika msimu wa 2013-14, tumemaliza vibaya katika nafasi tab saba, ambayo inamaanisha hatutashiriki michuano ya Ulaya.
"Kuwa na uhakika kila mmoja katika klabu anapambana kuhakikisha msimu ujao tunakuwa katika kiwango cha juu cha Manchester United.
"Tumefanya mabadiliko ya bench la Ufundi Aprili, tumefurahi kuwa na Ryan Giggs kwa kumalizia msimu vizuri. Kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu katika kupata kocha mpya na tarajia atatangazwa muda si mrefu,".
Louis van Gaal ndiye kocha anayetarajiwa kuichukua Manchester United baada ya Fainali za Kombe la Dunia atakapoiongoza kwa mara ya mwisho Uholanzi.
Jumatano Giggs alitua Uholanzi na akapigwa picha na inasemakana alikwenda kufanya mazungumzo na Van Gaal kwa niaba ya klabu.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago