KIUNGO Samir Nasri ameendeleza wiki nzuri za mafanikio katika soka, baada ya jioni ya leo kufanya kazi nzuri Manchester City ikicheza mchezo wa kirafiki na Al Ain katika ziara yake ya Falme za Kiarabu.
Mfaransa huyo atakwenda na kulala na tabasamu zuri baada ya kutengeneza mabao mawili katika ushindi wa 3-0 wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Hazza bin Zayed.
Anakwenda na mpira: Nyota wa Manchester City, Samir Nasri akimtoka beki wa Al Ain katika mchezo wa kirafiki leo
Tunakupenda: Shabiki huyo alishindwa kujizuia na kuvamia uwanjani kwenda kumbusu Samir Nasri
Akiwa na machungu ya kutemwa na kocha Didier Deschamps katika kikosi cha Ufaransa cha Kombe la Dunia, Nasri alipambana kuhakikisha anawaziba midomo wanaomkandia baada ya demu wake, kutweet matusi dhidi ya timu ya taifa.
Ameacha miguu yake izungumze, akiwapasia mipira ya kufunga Marco Lopes dakika ya 63 na Stevan Jovetic dakika ya 78 katika me chi ambayo wenyeji walibadilisha wachezaji 25.
Bao lingine la City lilifungwa na Hiwula kwa penalti dakika ya 89 katika mechi iliyohudhuriwa na watu 21,437. Al Ain ndiyo klabu yenye mafanikio zaidi kihistoria UAE na Jumapili itacheza Fainali ya Kombe la Rais.
Marcos Lopes akishangilia bao lake dhidi ya Al Ain
Mwenye timu: Mmiliki wa Manchester City, Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan akipiga makofi Uwanja wa Hazza bin Zayed leo
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago