ONAJINSI DIAMOND ALIVYONYAKUWA TUZO SABA KILIMANJARO MUSIC,HUKU MASHUJAA BENDI IKIWA NDIO BENDI BORA

Na Baby Akwitende, Dar es Salaam
MSANII wa muziki wa kizazi, Nassib Abdul 'Diamond Platnum' usiku wa kuamkia leo amevunja rekodi baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa tuzo saba tofauti katika tamasha la tuzo za muziki nchini mwaka huu 'Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014' lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Diamond ambaye nyota yake ya muziki ilianza kutamba alipotoa kibao cha Mbagala, mwaka huu amebebwa na wimbo uitwao Number One uliorekodiwa bure kwa mtayarishaji Sheddy Clever wa Burns Records.

Mwigizaji nyota Tanzania, Wema Sepetu akimpa tuzo mpenzi wake usiku wa jana ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam

Number One imetwaa tuzo sita ambazo ni pamoja na Wimbo bora wa mwaka, Wimbo bora wa Afro Pop, Mwimbaji Bora wa Kiume, Mtumbuizaji Bora wa Kiume wa Muziki, Mtunzi Bora wa Mwaka- Kizazi Kipya na tuzo ya Video Bora ya muziki ya mwaka.
Tuzo ya mwisho ambao Diamond ambaye alisindikizwa na rafiki yake wa kike, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ni ya Wimbo Bora wa Kushirikiana ambayo amefanya na Ney wa Mitego (Muziki Gani).
"Wallah sijui niseme nini, nimefurahi sana, napenda kumshukuru Sheddy Clever ambaye alinitengenezea hii nyimbo bure na mimi nilimuahidi nitaitendea haki, napenda kuwashukuru wadau wote wa muziki wanaoshabikia kazi zangu bila kumsahau Wema ambaye ananifanya naweza kutunga mashairi mazuri," alisema Diamond mara baada ya kupokea tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka kutoka kwa Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ndiyo wadhamini wakuu wa tuzo hizo, George Kavishe.
Wasanii wengine waliong'ara katika tuzo hizo ni pamoja na
Mzee Yusuph ambaye alipata tuzo nne ya Mwimbaji Bora wa Kiume- Taarab, Mtunzi Bora wa Mwaka (Taarab), Wimbo Bora wa Mwaka wa Taarab (Wasi Wasi Wako) na Jahazi ikitangazwa kuwa mshindi wa kikundi bora cha mwaka cha muziki huo wakati Lady Jay Dee alitwaa tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike- Kizazi Kipya na ya Wimbo Bora wa Zouk (Yahaya).

Watu wakifurahia shughuli


Kulia ni Baraka Shelukindo


Kulia ni Aggrey Marealle

Hata hivyo Mzee Yusuph, Lady Jaye Dee, Hassan Bichuka ambaye alishinda tuzo ya Heshima na Masoud Masoud (Taasisi iliyotoa mchango) hawakuwepo kupokea tuzo hizo ukumbini hapo.
Tuzo ya Wimbo Bora wenye Vionjo vya Asili ya Kitanzania ilichukuliwa na Bora Mchawi (Dar Bongo Movie), Wimbo Bora wa Kiswahili- bendi (Ushamba Mzigo), Wimbo Bora wa Reggae (Niwe na Wewe- Dabo), Wimbo Bora Afrika Mashariki (Jose Chamelleone), Wimbo Bora wa Hip Hop (Nje ya Box- Nick wa Pili ft Joh Makini na Gnako), Wimbo Bora wa R& B (Closer-Vanessa Mdee), Wimbo Bora wa Ragga/ Dance Hall (Nishai- Chibwa ft Juru) na Isha Ramadhani alishinda tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike -Taarab.
Isha pia alitwaa tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa Kike- Taarab, Jose Mara (Mwimbaji Bora wa Kiume wa bendi wakati kwa wanawake Luiza Mbutu wa African Stars 'Twanga Pepeta' aling'ara, Fid Q alishinda tuzo mbili ya Msanii Bora wa Hip Hop na Mtunzi Bora wa Mwaka wa muziki huo, Young Killer (Msodoki) alitwaa ya Msanii Bora Chipukizi anayeibukia, Ferguson (Rapa Bora wa Mwaka- bendi) huku Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka (Taarab) alikuwa ni Enrico.
Man Water wa studio ya Combination alishinda tuzo ya Mtayarishaki Bora wa Nyimbo wa Mwaka (Kizazi Kipya) na kwa upande wa bendi ilienda kwa Amoroso huku Mtunzi Bora wa Mwaka wa bendi aliyeshinda ni Christian Bella, bendi bora ya mwaka ni Mashujaa.
Tuzo hizo zilisindikizwa na burudani mbalimbali na baadhi ya waliofanya vizuri ni Diamond, Mwana FA ambaye alikuwa na wacheza shoo wamasai, Weusi Classic, Fred Saganda aliyetamba na Raphael, King of Routs ambaye alipiga kwa umahiri tarumbeta kwa kuimba nyimbo mbalimbali kwa ufanisi.
Naye Chamelleone wakati anapokea tuzo hiyo aliwashukuru Watanzania na wananchi wengine wa Afrika Mashariki kwa kumuunga mkono kazi zake ambazo nyingi anatumia lugha ya kiswahili.
"Mara ya kwanza kukutana na Rais Museveni (Rais wa Uganda) aliniuliza nimezaliwa Tanzania au Kampala, kwa sababu naimba sana kiswahili na hata wasanii wenzangu wananiuliza sana," alisema msanii huyo.





Diamond Platnum amedhihirisha kuwa yeye ni msanii mkali wa levo za kimataifa mara baada ya kuchukuwa tuzo saba katika Tuzo za Kilimanjaro 2014 (KTMA).


Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company