UN kutumia drones (ndege isiyokuwa na rubani) kudhibiti machafuko CAR

Umoja wa Mataifa umesema kuwa, unafikiria kutuma ndege zisizo na rubani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kudhibiti machafuko katika nchi hiyo. Herves Ladsons Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Operesheni za Kulinda Amani amesema kwamba, taasisi hiyo inajadili suala la kutuma ndege zisizo na rubani kwa lengo la kuchunguza matukio yanayojiri katika ardhi ya nchi hiyo yenye machafuko na kwamba kifaa hicho ni chenye faida katika maeneo kama hayo.

Hayo yanajiri huku Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati akieleza kusikitishwa na machafuko yanayoendelea nchini humo na kutoa wito wa kupelekwa haraka askari wa Umoja wa Mataifa. Andre Nzapayeke amesisitiza kwamba, wananchi na serikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wanajitahidi kufanya jitihada za kurejesha amani na usalama nchini humo. Askari 12,000 wa Umoja wa Mtaifa wanatarajiwa kuwasilia Bangui Septemba mwaka huu.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company