Indonesia inasema imekamata watu watano kwa tuhuma za kukusanya fedha za kuandikisha wanachama wapya kwa kundi la Islamic State.
Katika mkutano wa wanahabari Jumatatu, makamu mkuu wa polisi Jenerali, Badrodin Haiti, amesema watu hao watano walishikiliwa jumamosi katika vitongoji vya Jakarta.
Ameongeza pia maofisa waligundua hati za kusafiria kama passport, ticketi za ndege, simbu za mkononi kadhaa na fedha zilizo katika sarafu ya Indonesia na Marekani.
Polisi walikamata vitu hivyo pale walipovamia nyumba ya mmoja wa washukiwa hao.
Mapaka sasa watuhumiwa hawajapata fursa ya kujibu tuhuma zao hadharani.