Jeshi la Nigeria katika mji wa Bama katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria
Jeshi la Nigeria limesema limeurejesha mji wa Bama uliko kaskazini mashariki mwa Nigeria kutoka kwa wapiganaji wa Kiislam wa kundi la Boko Haram.
Wapiganaji wa Boko Haram walikuwa wakiudhibiti mji wa Bama, ambao ni wa pili kwa ukubwa katika jimbo la Borno tangu mwezi Septemba mwaka jana.
Mike Omeri, msemaji wa Rais Goodluck Jonathan, amethibitisha kuwa majeshi ya Nigeria yaliingia Bama.
Alipoulizwa na BBC ni kwa nini imechukua wiki mbili kuutwaa tena mji huo kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge, amesema jeshi lilikosa zana muhimu.
CHANZO BBC SWAHILI
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago