SENTESI 11 ZA ZITTO KABWE KENYE KIPINDI CHA DAKIKA 45 ITV JANA

Ni mengi ambayo yamesikika kuhusu Mbunge Zitto Kabwe siku za hivi karibuni, mojawapo ni ishu ya Mbunge huyo kusimamishwa Uanachama wa CHADEMA na pia akaamua kwenda kuongea na Wapigakura wake kwamba hatogombea tena nafasi hiyo.

Huenda kuna vitu hukuwahi kumsikia akizungumzia, mojawapo ni ishu ya usalama wake; “Suala la usalama sina tatizo kabisa kwa sababu ninachokifanya ni majukumu ya Kikatiba.. Wananchi wanachagua kundi la Wabunge 350 kwa ajili ya kazi tatu.. uwakilishi, kutunga Sheria na kuisimamia Serikali.. Hamjawahi kunisikia nalalamika kuhusu usalama, likitokea limetokea huwezi jua binadamu wanapanga nini…”

Zitto Kabwe anazungumzia miaka miwili ambayo ilikuwa migumu sana kwake kwenye siasa; “Kwanza 2007 wakati nimetoa hoja ya BUZWAGI.. Kipindi kile ilikuwa ni vigumu sana kwa Mbunge kusimama na kumwambia Waziri wa Serikali kamba umesema uongo.. Nikasimamishwa Ubunge kwa miezi minne..“

2014 pia ulikuwa ni mwaka mgumu na una sababu mbalimbali. Kwa mara ya kwanza nilijikuta nakwenda Mahakamani kwa ajili ya kutetea haki yangu kuhusiana na uanachama wangu kwenye chama.. Lakini ndio mwaka huo huo ambao nikawa na hoja nzito sana kwenye Bunge, hoja ya Escrow..“– Zitto KABWE.

Hii ni sehemu ya mahojiiano ya Mbunge huyo kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITVkilichoruka leo March 16.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company