Ndege ya Ujerumani yaanguka na kuuwa abiria 150

Eneo lililotokea ajali ya ndege ya Germanwings kwenye milima ya French Alps, Machi 24, 2015.
Waziri wa usafiri nchini Ufaransa, Alain Vidalies alisema jumanne kwamba hakuna mtu yeyote aliyenusurika kati ya abiria 150 waliokuwemo ndani ya ndege aina ya Airbus A320 ambayo ilipata ajali katika milima ya French Alps.

Bwana Vidalies alisema ujumbe wa dharura ulisikika kutoka ndege ya Germanwings ikitokea Barcelona, Spain kuelekea Dusseldorf, Ujerumani muda wa saa 10.47 asubuhi kwa saa za huko kiasi cha dakika 52 baada ya kuruka ikiwa imevuka eneo moja dogo lenye theluji huko kusini-mashariki mwa Ufaransa.

Ishara hiyo ya matatizo ilionyesha ndege ilikuwa kwenye kiwango cha futi 5,000 katika hali isiyo ya kawaida, alisema na kisha ilipata ajali muda mfupi baadaye.
Rais wa Ufaransa, France Hollande

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande alisema watu waliofariki ni pamoja na raia wa Ujerumani, Spain na pengine wa-Uturuki. Bwana Hollande alisema hawezi kuthibitisha kwamba hakuna raia yeyote wa Ufaransa aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo. “Ni janga ndani ya ardhi yetu” kiongozi huyo wa Ufaransa alisema.

Bwana Hollande alimpigia simu Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel kutoa rambi rambi zake. Msemaji wake alisema kuwa bibi. Merkel alishtushwa sana na tukio hilo na aliakhirisha miadi yake yote ya siku hiyo.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Spain, Mariano Rajoy alisema kwenye ujumbe wa Twitter kuwa alishtushwa na ajali ya ndege kwenye milima ya Alps. Ni janga. Tunashirikiana na maafisa wa Ufaransa na Ujerumani katika kufanya uchunguzi.

Mfalme wa Spain, Felipe alikuwa kwenye ziara ya kiserikali kuelekea Paris wakati ajali ikitokea lakini alisitisha safari yake na kurejea nyumbani.
Hakuna taarifa za kuwasili ndege 4U 9525

Ndege ya Germanwings 9525 ilikuwa imebeba abiria 144 na wafanyakazi sita. Maafisa walisema mabaki kutoka ajali ya ndege yameonekana na helikopta katika eneo moja dogo ambalo itakuwa vigumu kwa wafanyakazi wa utafutaji kufikia.

“Ni eneo ambalo lina theluji, magari hayapitiki”, alisema Vidalies.

Germanwings ni ndege ndogo ya shirika la ndege la Lufthansa lenye makao makuu yake Ujerumani. Ndege A320 ambayo ilipata ajali ilikuwa ikihudumu kwa miaka 24 na ilikuwa moja ya ndege za biashara zinazofahamika mno.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company