Shambulio la bomu katika peninsula ya Sinai
Wapiganaji wengi wa Kiislam wa kundi la Islamic State wameripotiwa kuuawa katika mapigano makali kati ya majeshi ya usalama ya Misri na kikundi hicho katika peninsula ya Sinai, kaskazini mwa Misri. Mapigano yalidumu kwa saa kadha kuzunguka mji wa Sheikh Zuwaid, kwa serikali kupeleka ndege na helikopta za kivita.
Mbali na kuuawa kwa wapiganaji wa Islamic State, wanajeshi na raia ni miongoni mwa waliopoteza maisha.
Habari kutoka mjini Cairo, Majeshi maalum ya usalama ya Misri yalizingira jengo moja na kuwaua wafuasi tisa wa kikundi cha Muslim Brotherhood. Wizara ya mambo ya ndani imesema watu hao walishukiwa kupanga mfululizo wa mashambulio. Kikundi cha Muslim Brotherhood kimesema wafuasi wake tisa waliuawa kikatili na kimewataka wafuasi wake kufanya maasi dhidi ya Rais Abdel-Fattah el-Sisi.
Wapiganaji wa Islamic State wamekuwa pia wakiendesha mashambulizi katika nchi za Syria na Iraq kwa lengo la kuzitawala nchi hizo.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago