Marekani na Cuba kufungua balozi zake.

Mpango huo wa mwisho utatekeleza ahadi ya wapinzani hao wa vita baridi waliyoitoa takriban miezi sita iliyopita wakati rais Obama na rais wa CUBA Raul Castro walipotangaza kufunguliwa kwa historia ya kidiplomasia. viongozi hao wawili walikutana huko Panama mwezi April.
Bendera ya Cuba ikipepea .

Utawala wa rais Obama jumatano utatangaza makubaliano yaliyofikiwa na CUBA kufungua tena balozi zake na kurejesha uhusiano wa kidemokrasia uliokuwa umeharibika kwa miaka mingi.

Rais Barack Obama yupo Washington, na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry yuko Vienna kwa ajili ya mazungumzo ya program za nyuklia za Iran , wote wataeleza juu ya suala hilo, alisema afisa mwandamizi wa serikali ya Marekani. Tangazo kama hilo linatarajiwa kutolewa pia na uongozi wa kikomunist wa serikali ya CUBA.

Mpango huo wa mwisho utatekeleza ahadi ya wapinzani hao wa vita baridi waliyoitoa takriban miezi sita iliyopita wakati rais Obama na rais wa CUBA Raul Castro walipotangaza kufunguliwa kwa historia ya kidiplomasia. viongozi hao wawili walikutana huko Panama mwezi April.

Kerry anatarajiwa kwenda havanna katika wiki ya Julai 20 kwa ajili ya sherehe ya kupandishwa bendera ya kufunguliwa kwa ubalozi wa Marekani huko. Ikulu ya marekani- white house itatangaza muda rasmi.

Nchi zote mbili sasa zinaweza kuboresha ushawishi wake Havanna na Washington katika balozi hizo, ambapo mabalozi wake wanatarajiwa kuteuliwa hapo baadae. Wizara ya mambo ya nje ya marekani lazima ilipe bunge taarifa ya siku 15 kabla ya kufungua ubalozi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company