Jenerali Nshimirimana auwawa

Watu waliokuwa na bunduki wamemuuwa mkuu wa usalama wa zamani wa Burundi na mshauri mkubwa wa Rais Pierre Nkurunziza.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema Jeneral Adolphe Nshimirimana alikufa pale gari lake liliposhambuliwa katika mji mkuu, Bujumbura.

Umoja wa Ulaya umesema mauaji yake yamezidisha wasiwasi, na kwamba juhudi za upatanishi lazima zianze tena.

Burundi imepita katika miezi kadha ya ghasia baada ya Rais Nkurunziza kuania na kushinda muhula wa tatu wa uongozi.

Inafikiriwa kuwa Jenerali Nshimirimana bado alikuwa na mchango mkubwa katika usalama, hata baada ya kutolewa kuwa mkuu wa usalama nchini Burundi.

Muandishi wa habari wa Ufaransa ambaye alipiga picha za pahala jenerali huyo aliposhambuliwa, alikamatwa na kupigwa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company