Naibu Waziri wa Kazi na Ajira , Dk. Makongoro Mahanga Atangaza Kuihama CCM......Asema Atahamia CHADEMA

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Segerea anayemaliza muda wake,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga, ametangaza kuihama CCM na kuhamia CHADEMA kutokana na kutokuwepo Demokrasia ya Kweli ndani ya CCM.

Dr. Mahanga ambaye ni Mbunge anayemaliza muda wake kwenye Jimbo la Segerea kwa tiketi ya CCM ametangaZA azma hiyo leo mchana baada ya rufaa yake ya kupinga ushindi wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kipawa mama Kivela kutupiliwa mbali na Ofisi ya CCM mkoa wa Ilala.

Duru za Kisiasa zinasema kilichomponza Dr. Mahanga ni kitendo chake cha yeye kuhusika katika mpango wa kumnadi Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kwenye nafasi ya Urais wa CCM, ambaye kwa sasa ametangaza kugombea urais kupitia Chadema.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company