Ghasia za kisiasa zinaendelea nchini Burundi hata baada ya uchaguzi mkuu kufanyika
Maafisa nchini Burundi wanasema kiongozi mmoja wa chama tawala nchini humo alishambuliwa na kuuwawa katika mji mkuu, Bujumbura. Huyu ni kiongozi wa tatu kushambuliwa katika muda wa siku tatu.
Maafisa hao walieleza Come Harerimana, rais wa chama cha CNDD-FDD katika wilaya ya Kanyosha alikuwa akielekea ofisini akiwa nyuma ya pikipiki wakati umati ulipomrushia mawe. Bwana Harerimana alivutwa kutoka kwenye pikipiki na kupigwa risasi.
Burundi hivi sasa inashuhudia ghasia mbaya za kisiasa tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2005. Ghasia hizi zilianza mwezi April wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwa atawania muhula wa tatu madarakani hatua ambayo wapinzani wake na mataifa ya magharibi walisema inakiuka katiba na mkataba wa amani wa Arusha ambao ulipelekea kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Uchaguzi nchini Burundi
Rais Nkurunziza alitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa kiti cha urais uliofanyika hapo Julai 21 kufuatia miezi kadhaa ya maandamano mitaani na jaribio la mapinduzi lililoshindikana.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago