Ajali iliyotokea jana katika kijiji cha Mavuji wilayani Kilwa imesababisha vifo vya watu watano wa familia moja ambapo walikuwa wanatoka kuwazika ndugu zao wawili juzi mjini Lindi baada ya marehamu hao kupata ajali.
Waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na Bi Saida ambaye ni mama Mzazi wa Marehemu, Shiraz Jack Magongo aliezikwa Juzi, Shirin Jack Magongo ambae ni Mama Mzazi wa Marehemu Samia (MRS Lupanda) pamoja na Marehemu Shiraz.
Marehemu wa awali walipata ajali ambayo ilitokea majuzi katika Kijiji Cha Chipite.(P.T)
Marehemu Mwingine ni Ajira Shiraz Jack Magongo Nargis ambaye ni dada yao wa mama mkubwa na Mdogo ambaye kwa waliokuwa Lindi ndiye mmiliki wa nyumba ya Gift Guest na walio Dar yupo Livingstone Str maarufu kwa uuzaji wa chumvi, pamoja na Meja Hussein Bhatia ambae ndie alikuwa dereva wa gari hilo ambaye alifariki baadaye.
Maiti ya marehemu Bi Saida, Shirin na Nargis zinatarajia kuzikwa Dar huku maiti ya Marehemu Meja Hussein Bhatia na Ajira Shiraz ikiwatarajiwa nayo kuzikwa mkoani Lindi.
Katika ajali hiyo dada mkubwa wa marehemu Shiraz na Shirin, Yasmin Jack Magongo walikimbizwa katika hospitali jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Mwingine ambaye ni Salma Mohamed Zaid, mtoto wa Mama Malaika Hotel (mama mzazi wa marehemu Ajira Shiraz aliyefariki katika ajali hiyo) ametoka salama katika ajali hiyo.
Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni kutanda kwa moshi barabarani na gari aina ya Noah T594 DDH lililosababisha watu hao kufariki dunia kuligonga basi la SB lililokuwa limesimama kando ya barabara.
via Juma Mtanda
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago