Wapiga kura wasajiliwa Jamhuri ya Africa ya Kati

Jenerali Babacar Gaye, mwakilishi wa umoja mataifa Jamhuri ya Africa ya Kati .
     Kiongozi wa ujumbe wa umoja wa mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya kati amesema kuwa usajili wa wapiga kura kwa sababu ya uchaguzi ujao unaendelea na kwamba karibu theluthi moja ya wapiga kura wamejiandikisha kufikia sasa.

Babacar Gaye jumatano ameambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba karibu wapiga kura milioni moja wamejiandikisha hasa katika mji mkuu Bangui na shughuli hiyo inaendelea kwenye sehemu zingine za nchi.

Amesisitiza umuhimu wa kuandikisha takriban raia 400,000 ambao wamekuwa wakimbizi tangu vita vya kijamii ndani ya nchi vilipozuka baina ya wanamgambo kiislamu na wakristo 2013.

Gaye amesema kuwa kati ya asilimia 75 na 85 ya wakimbizi hao ni waislamu na kushiriki kwao kweye uchaguzi ni muhimu kwa kuleta uuwiano.

Amesema kuhusika kwao kwenye uchaguzi huu ni hatua ya ziada kuelekea mapatano na kurejesha tena uhusiano katika jumuiya nchini.

Ameelezea kwamba mahakama ya katiba nchini humo imeweka bayana kuwa wakimbizi wana haki ya kushiriki kwenye uchaguzi.

Gaye amesema kuwa kuhusishwa kwa kila mmoja ni muhimu kama ishara ya uchaguzi sahihi.

Kura ya maoni ya katiba imepangwa kufanyika oktoba 4, 2015 wakati duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na bunge ukipangwa kufanyika oktoba 18. Duru ya pili inatarajiwa kufanyika novemba 22.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company