Muasisi wa Tanu na baadaye CCM, Mzee Peter Kisumo (pichani) amefariki dunia.
Mwanasiasa huyo mkongwe nchini ambaye aliwahi kushika nyadhifa kadhaa katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, alifariki Dunia jana saa moja usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mtoto wa marehemu, Michael Kisumo alilithibitishia gazeti hili jana juu ya kifo cha baba yake akisema kilitokana na maradhi ya figo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
“Tulikuja hapa Muhimbili kwa ajili ya mzee kufanyiwa dialysis (usafishaji damu katika figo) sasa ikajitokeza complication (utata) akaanza kuharisha damu,” alisema.(P.T)
Michael alisema baba yake alilazwa wodi ya kawaida juzi ili jana apatiwe tiba hiyo kabla ya hali yake kubadilika ghafla.
“Daktari wake alipokuja leo (jana) na kumwangalia aliagiza atolewe wodi ya kawaida ahamishiwe ICU lakini ilipofika saa moja usiku akatutoka” alisema Michael.
Kifo cha mwanasiasa huyo kimekuja takribani mwezi mmoja tangu arejee kutoka India ambako amekuwa akienda mara kwa mara kuchunguzwa afya yake.
Hali ya ugonjwa wake huo ilifikia katika kiwango cha juu na kulazimika kufanyiwa uchujaji wa figo mara tatu kwa wiki kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.
Kisumo aliwahi kuwa mmoja wa mameneja wa kampeni wa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2005 akisimamia kanda ya kaskazini iliyojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga.
Mbali ya kuwa waziri, aliwahi pia kuwa mkuu wa mkoa na mdhamini wa CCM.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago