Israel: Myahudi mwenye msimamo mkali awekwa kizuizini

Serikali ya Israel imeamua kutekeleza sera yake ya kukabiliana na Wayahudi wenye msimamo mkali kufuatia mfululizo wa majanga, ikiwa ni pamoja na uchomaji wa nyumba katika kijiji kimoja cha Palestina kiliyosababisha kifo cha mtoto mchanga.
REUTERS/Abed Omar
             Na RFI
Serikali ya Israel ilikuwa ameahidi kuwachukulia hatua kali wayahudi wenye msimamo mkali. Katika masaa 48, Wayahudi kadhaa wenye msimamo mkali wamekamatwa.


Na mmoja wao amewekwa kizuizini, Jumanne Agosti 4, kwa kipindi cha miezi sita. Hadi sasa, hatua hii iiliokua ikishutumiwa na mashirika yanayotetea haki za binadamu, ilikua ikitumika hasa kwa Wapalestina. Hii ni mara ya kwanza raia wa Israel kukabiliwa na hatua.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Jerusalem, Michel Paul, waziri wa ulinzi wa Israel Moshe Yaalon ametia saini kwenye sheria ya kuwaweka kizuizini watu wenye msimamo mkali katika mfumo wa sera ya kukabiliana na wahalifu uliopitishwa na serikali ya Israel.

Hatua inayomuhusu Mordechai Mayer, mlowezi wa Israel aliyekamatwa kwa sababu ya "ushiriki wake katika vurugu na mashambulizi ya kigaidi katika siku za hivi karibuni," kulingana na taarifa ya wizaraya hiyo ambayo haikuweka bayana kama alihusika moja kwa moja kwa uhalifu wa kikatili wa kuchoma moto nyumba moja katika kijiji kimoja cha Palestina kaskazini mwa Cisjordania ambacho kilisababisha kifo cha mtoto mchanga wa Kipalestina wa miezi 18.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni ya Israel, Wayahudi wengine wawili wenye msimamo mkali pia wanaweza kuwekwa kizuizini, utaratibu uliozua utata ambao ulianza katika enzi za mamlaka ya Uingereza kwa Palestina na ambao umekua ukitumika dhidi ya Wapalestina. Utaratibu huo unapelekea kuwazuia kizuizini watu bila hata hivyo kushitakiwa au kuhukumiwa kwa vipindi mbadala vya miezi sita.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company