Image copyrightAFPImage captionUpinzani DRC
Vyama kadhaa vya upinzani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo vimeitisha maandamano katika mji mkuu wa taifa hilo Kinsasha dhidi ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais uliotarajiwa mwezi Novemba mwaka 2016.
Wiki iliopita ,mahakama ya kikatiba nchini humo ilitaka siku ya uchaguzi huo kuangaziwa upya ,hatua ambayo wapinzani wanasema ni ya kutaka rais Joseph Kabila kusalia mamlakani zaidi hata baada ya kukamilika kwa muda wake uliowekwa kikatiba.
Mabango yaliobebwa na vyama hivyo yalisoma ''mabadiliko ya uongozi ni sharti yafanyike''.Image copyrightImage captionDrc
Maandamano ya kupinga kucheleweshwa kwa uchaguzi huo yalizua ghasia mnamo mwezi Januari na kusababisha vifo vya takriban watu 36.
Bwana Kabila amekuwa madarakani tangu babaake aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo auwawe mwaka 2001.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago