Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira dakta BINILITH MAHENGE amewataka waandishi wa habari kuhabarisha umma kuhusu utunzaji wa tabaka la ozone
Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira dakta BINILITH MAHENGE amewataka waandishi wa habari kuhabarisha umma kuhusu utunzaji wa tabaka la ozone.Akizungumza na waandishi wa habari Mhandisi MAHENGE amezitaja njia za kuhabarisha umma kuhusu tabaka la ozon kuwa ni pamoja na kuepuka kuingiza nchini gesi zilizopigwa marufuku, na kuepuka kutumia vifaa vya zimamoto vyenye kemikali zinazoweza kuharibu tabaka la ozon
Aidha Mhandisi MAHENGE amesisitiza wananchi kuingiza vipodozi na bidhaa rafiki kwa tabaka la ozone.
Siku ya kimataifa ya tabaka la ozone huadhimishwa kila tarehe 16 September ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu yake ni “ MIAKA THELATHINI YA KUREJESHA TABAKA LA HEWA YA OZONE KWA PAMOJA