Wanajeshi hao wa Afrika Kusini wanadaiwa kuhatarisha usalama wa wanajeshi wengine
Wanajeshi hamsimi wa Afrika Kusini waliokuwa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kinacholinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Monusco) wameagizwa kurejea nyumbani.
Viongozi wa jeshi nchini Afrika Kusini wamesema wanajeshi hao wataadhibiwa kwa kuwa wamekiuka maadili ya utendakazi.
Taifa hilo lina takriban wanajeshi 1,400 wanaohudumu Congo, wakijaribu kusaidia kukomesha vita mashariki mwa DR Congo.
Baadhi ya wanajeshi wanadaiwa kuhatarisha usalama wa wanajeshi wengine wa UN nchini DR Congo.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago