AL Libi akana kuhusika na mashambulizi ya kigaidi


Mtuhumiwa wa ugaidi AL Sanusi Al Libi
Na Martha Saranga Amini

Mtuhumiwa wa ugaidi na anayedaiwa kuwa mshirika wa karibu wa mtandao wa kigaidi duniani wa Al-Qaeda raia wa Libya, Anas al-Libi hapo jana amepandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza na kukana mashtaka yanayomkabili.

Akionekana mwenye kujiamini, Anas al-Libi alimwambia jaji anayesikiliza kesi hiyo kwenye mahakama ya mjini New York, kuwa hana hatia dhidi ya tuhuma za kuhusika na tukio la ulipuaji wa balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998.

Anas al-Libi amesomewa zaidi ya mashtaka sita ikiwemo kupanga njama za mauaji, utekaji nyara, mauaji ya halaiki pamoja na uharibifu wa mali na majengo ya usalama ya Marekani, mashtaka ambayo yote amekana kuhusika nayo.

Hata hivyo hatua ya serikali kumfikisha mtuhumiwa huyo wa ugaidi kwenye mahakama ya kiraia mjini New York imezua mjadala mkubwa miongoni mwa wananchi ambao wanataka mtuhumiwa huyo ashtakiwe kwenye mahakama ya gereza la Guantanamo kutokana na makosa aliyotenda.

Anas al-Libi alikamatwa na makomandoo wa Marekani kwenye viunga vya mji wa Tripoli nchini Libya octiber 5 mwaka huu na kusafirishwa hadi mjini New york ambako alifunguliwa kesi mwaka 2000.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company