Naibu Rais wa Kenya Bw William Ruto jana aliitaka mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC kusimamisha kesi inayomkabili yeye na Rais Uhuru Kenyatta hadi baraza la usalama la Umoja wa ataifa litakapotoa uamuzi. Katika taarifa iliyotolewa mjini Nairobi na ofisi yake, Bw Ruto pia ameishutumu mahakama hiyo kwa kushindwa kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma zinazowakabili, na kusema njia inayotumiwa na mahakama hiyo kutafuta ushahidi inaonesha kuwa ina lengo la kuwanunua na kuwahonga mashahidi. Kauli ya Bw Ruto imekuja wakati Umoja wa Afrika umelitaka baraza la usalama kuacha kesi dhidi ya viongozi wa Kenya.
Wakati huohuo Rais Paul Kagame wa Rwanda ameipinga mahakama hiyo kwa kusema inaendesha kesi kwa ubaguzi. Amesema msimamo wa Rwanda kuhusu mahakama hiyo hautokani na matokeo ya kesi ya viongozi wa Kenya, bali ulifikiwa miaka 10 uliyopita, ndio maana Rwanda haikusaini mkataba wa kujiunga na mahakama hiyo.
www.hakileo.blogspot.com