Hiki ndicho alichokijibu Zitto Kabwe baada ya tamko la Dr.Slaa

Zitto Kabwe leo amefanya mkutano wa 3 ndani ya Mkoa wa Kigoma,mikutano hii ilianza siku ya Jumamosi kwa sehemu ya Mwandiga mahali alipozaliwa na kukulia,Kasulu ilikua jana na leo kafanya Kigoma mjini eneo la Mwanga kwenye uwanja wa Community Centre.

Mkutano ulianza sa 10 kiitifaki ulitanguliwa na viongozi wa Chadema wa mkoa,kisha Zitto Kabwe kupanda Jukwaani na moja kati ya vitu alivyovizungumzia ni kuhusu tamko la Dr.Wilbroad Slaa alipokuwa kwenye mkutano wake wa Kuimarisha chama uliofanyika Igunga Mkoani Tabora,

Dr.Slaa alizungumzia kuhusu mikutano anayoifanya Zitto Kabwe kuwa si halali yeye anatakiwa kufanya kwenye jimbo lake tu ambalo ni Kigoma Kaskazini hiki ndicho alichokizungumza kufuatia tamko hilo la Dr.Slaa ‘Sasa jana Katibu Mkuu kasema Kwanini nafanya ziara zaidi ya Kigoma Kaskazini siruhusiwi kwenda sehemu nyingine yoyote baada ya kusikia yale mapokezi ya Kasulu’.

‘Mimi nawaambia katiba ya Nchi hii inaniruhusu kwenda mahali kokote,sehemu yoyote nchi hii kwa mujibu wa katiba maana mimi bado Mbunge kama wamenifukuza waseme kuwa wamenifukuza lakini kama hawajanifukuza mimi bado mbunge’.

‘kwa hiyo nitaenda Kigoma Kaskazini,nitaenda Kigoma Kusini,nitaenda Kasulu,nitaenda Kigoma Mjini kuhutubia Wananchi na siyo hivyo tu nitaenda Mpanda,nitaenda Tabora,nitaenda Shinyanga,nitaenda Mwanza nitaenda hadi Arusha na hakuna mtu wa kunizuia’.

Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company