MWAKA 2014 utaanza kwa maumivu kwa Watanzania baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuridhia maombi ya Shirika la Umeme (TANESCO) kupandisha gharama za matumizi ya umeme mara mbili ya maombi ya shirika hilo.
Katika maombi ya TANESCO iliyoyawasilisha Oktoba 11, mwaka huu, ilipendekeza kuongeza bei kwa awamu ambapo asilimia 67.87 kuanzia Oktoba mosi, 2013, asilimia 12.74 kuanzia Januari Mosi, 2014 na asilimia 9.17 kuanzia Januari Mosi, 2015.
Pia shirika hilo liliomba kuidhinishiwa kwa kanuni ya kurekebisha bei ya umeme kulingana na mabadiliko ya bei za mafuta, mfumko wa bei na mabadiliko ya thamani ya shilingi ya Kitanzania pamoja na kuidhinishiwa viwango vya gharama za kuunganisha umeme vinavyozingatia ruzuku inayotolewa na serikali na kuidhinishiwa kwa tozo mbalimbali kwa huduma zitolewazo na shirika hilo.
Akisoma taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Haruna Masebu Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi wa Uwura Felix Ngamlagos alisema kutokana na maombi hayo EWURA imeridhia na kupandisha kiwango cha umeme.
Alielezea mchanganuo wa makundi ya walaji na bei zake, alisema kuna kundi D1 la wateja wadogo wa majumbani hasa vijijini ambao hutumia wastani wa uniti 75 badala ya ile ya 50 kwa mwezi na watalazimika kulipia kiwango cha sh 100 sawa na ongezeko la asilimia 40.
Kundi la T1 ni la watumiaji wakubwa wa umeme wa majumbani, biashara ndogo ndogo, ikiwa ni pamoja na mashine za kukoboa na kusaga nafaka, taa za barabarani mabango ambapo bei iliyoidhinishwa ni sh 306 kwa uniti moja ikiwa ni ongezeko la sh 85 ya bei ya sasa huku TANESCO ikiwa ilipendekeza bei ya sh 131.
Katika kundi T2 la watumiaji umeme wa kawaida ambao hupimwa katika msongo wa volti 400 na matumizi yao ya wastani kwa mwezi ni zaidi ya uniti 7,500.
Kundi hili linawagusa wafanyabiashara wakubwa, viwanda vya kati na bei ya nishati iliyoridhiwa ni sh 205 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la sh 73 ya bei ya sasa huku TANESCO ikiwa imeomba iidhinishiwe sh 145.
Katika kundi la T3-MV hili ni maalumu kwa wateja wakubwa wa viwanda vikubwa waliounganishwa katika msongo wa kati ambapo EWURA imewaidhinishia bei ya nishati kwa kiwango cha sh 166 kwa uniti moja sawa na ongezeko la sh 45 ya bei ya sasa huku TANESCO wakiwa walipendeza uniti moja wauze kwa sh 148.
Katika kundi la T3-HV la wateja wakubwa waliounganishwa katika msongo wa juu wenye voti 66,000 na zaidi ikiwa ni pamoja na ZECO Bulyanhulu na kiwanda cha Twiga bei iliyoidhinishwa ni sh 159 kwa uniti moja sawa na ongezeko la sh 53 la bei ya sasa huku bei hizo zikitakiwa kudumu hadi mwaka 2016.
“Bei ya umeme itakuwa inarekebishwa baada ya miezi mitatu kulingana na mabadiliko ya viwango na bei za mafuta, mfumko wa bei, mabadiliko ya thamani ya fedha na upatikanaji wa ruzuku toka serikalini.
“TANESCO pia inatakiwa kutekeleza miradi ya uwekezaji iliyoainishwa kwa kutumia fedha zitakazokusanywa kutokana na bei iliyoidhinishwa, EWURA inaweza kurekebisha bei ya umeme ya TANESCO mwisho 2014 au 2015 kama shirika hilo litashindwa kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya shirika,” alisema Ngamlagos.
Hata hivyo aliendelea kufafanua kuwa bei hizo zimepitishwa na bodi ya wakurugenzi wa EWURA katika kikao chake cha Desemba 10 mwaka huu baada ya kufanya uchambuzi kama kanuni na sheria zilivyoelekeza.
Alieleza uchambuzi huo pia ulifanyika kifedha na kiufundi kubaini uwezo wa TANESCO katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku, kwa kuangalia utendaji katika miaka mitano iliyopita na katika miaka mitatu ijayo na kubaini kuwa shirika lina hali mbaya ya kifedha.
Shirika linapata hasara iliyoongezeka kutoka sh bilioni 47.3 mwaka 2010 hadi bilioni 223.4 kwa mwaka 2012.
Kutokana na kuporomoka kwa shirika hilo katika masuala ya fedha, imelifanya kuwa na malimbikizo ya madeni yaliyofikia kiasi cha sh bilioni 456.8 Novemba 22 mwaka huu.
Naye Meneja Uchambuzi wa Masuala ya Fedha wa EWURA, Anastas Mbawala alisema pamoja na maamuzi hayo bodi ya wakurugenzi ililiagiza shirika hilo kuzalisha umeme kwa kutumia mitambo ya gharama nafuu na kuwasilisha ripoti kwa mamlaka kila mwezi.
Pia alisema shirika hilo linatakiwa kuwasilisha ripoti kila baada ya miezi mitatu kuhusu viashiria vya takwimu za ubora wa uhakika wa umeme.
Pia wametakiwa kuwahamisha wateja walio katika kundi D1 kwenda T1 endapo matumizi yao kwa mwezi yatazidi uniti 75 kwa miezi mitatu mfululizo.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago