MTANGAZAJI WA REDIO METRO FM 96.4 MWANZA AMEFARIKI DUNIA,HUZUNI MAJOONZI VYATAWALA MWANZA,KUZIKWA LEO.

Meneja wa Metro Fm Alex Ngusa (kulia) ameongoza kikao cha watumishi wa kittuo hicho kutoa taarifa na utaratibu wa jinsi ya kujipanga na kwaajili ya kushiriki taratibu zote hata kumpumzisha katika nyumba ya milele mtumishi mwenzao.



Marehemu Dj Alex anatarajiwa kuzikwa leo (jumatano) nyumbani kwao wilayani Bunda mkoani Mara.

Kutoka kulia ni Dj Victor, Tommy Alphonce na Jackob Usungu ambaye alikuwa akishirikiana na marehemu kufanya kipindi kimoja cha muziki wa Afrika kilichokuwa kikiruka majira ya jioni kikitikisa hasa.


Simanzi kubwa imewakumba watangazaji, wanahabari na wasikilizaji wa kituo cha radio Metro Fm ya jijini Mwanza mara baada ya kuondokewa na mmoja kati ya mfanyakazi mwenzao aliyetambulika kwa jina la DJ Alex.
Dj Alex alifariki dunia juzi akiwa ni mmoja kati ya abiria wa basi la kampuni ya Luhuye lililokuwa likitokea Sirari Mkoani Mara Kwenda Kahama kupata ajali katika eneo la Masanza Kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company