Kwa kweli kumekuwa na wimbi la mauwaji ya watu hawa wenye ulemavu wa ngozi hapa nchini tangu mwaka 2006 kuku tatizo hili likifanyika sana kwenye mikoa ya kanda za ziwa.
Katika hili watu wengi wamekuwa wakitupa lawama zao kwa serikali lakini yote katika yote serikali inasitahili kulaumiwa ila jambo hili ni swala mtambuka kwa hiyo sio serikali tuu inayositahili kubeba msalaba huu bali hata jamii na familia.
Siku chache zilizopita mbunge mmoja alikuwa akihojiwa kwenye kipindi fulani cha redio katika redio ya Clous fm yenye makazi yake jijini Dar es salaam ,alisema ya kwamba unyanyapa upo hadi bungeni kwani yeye ni mbunge na hapo alipo wabunge wenzake wananyanyapaa wakati mwingine hata hawataki kumpa mkono na akiwasalimia hawaitikii salamu yake na chakushangaza hata mawaziri nao wamo katika jambo hilo.
Pia anadai ya kwamba tatizo ama wimbi hili linaendelea kwa saababu serikalini kuna watu ambao wanapuzia swala hili kwa kuendelea kukumbatia mila potofu.
Labla niwakumbushe wale vijana wenzangu waliuopitwa na historia kidogo ya kwamba tatizo hili ni la bara la Afrika kwani hata kule nchini Naijeria na kungineko lilikwepo na mfano mzuri ni kwamba machifu wakiafrika na viongozi wakale ikiwemo pia nchini Misiri Mafarao walikuwa wakizikwa na watu wenye ulemavu huu wangozi wakiwa hai.
Na wengine walikuwa wakiuwawa nalikitokea hilo basi husemekana eti ya kwamba watu hao hawafi badala yake hutoweka.
Tureje kwenye kiini cha safu hii,Fikra za leo zinaitaka serikali na jamii na familia kwa ujumla kushikama na wote kutimiza wajibu wao katika hili kwani zipo familia nyingine ambazo wazazi ama ndugu huwatenga watu hawa na wakati mwingine huwapa ulinzi afifu na wengine wanakuwa hata tayari kushiriki katika kuwauza wakiwaita ni dili,mimi na wewe tukishikamana tunaweza kutokomeza ukatili huu ambao kwa hakikia unasononesha sana.