Usitishaji wa mapigano utaanza kutekelezwa mashariki mwa Ukraine tarehe 15 15 Februari,kwa mujibu wa viongozi wa Urusi na Ukraine.
"Tumeweza kukubaliana masuala ya msingi," Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema baada ya mazungumzo marefu na rais wa Ukraine, Petro Poroshenko, pamoja na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani.
Rais Francois Hollande wa Ufaransa amesema "mkataba madhubuti" umefikiwa, japokuwa bado kuna kazi ya kufanya.
Maelfu ya watu wameuawa katika mapigano mashariki mwa Ukraine.Silaha zilizotumika katika mgogoro wa mashariki mwa Ukraine
Mkutano wa viongozi hao nchini Belarus - ambao umedumu kwa saa 17- ulilenga kutafuta ufumbuzi wa kusitisha mapigano, kuondolewa kwa silaha kali kutoka eneo la mgogoro na kuanzisha ukanda huru usio wa kivita mashariki mwa Ukraine.
Bwana Putin amesema mkataba huo pia umeweka mpango wa kuondoa silaha kubwa kutoka eneo hilo. Waasi wa Ukraine wanaoungwa mkono na Urusi wamekubali mkataba huo.
Bwana Hollande amesema yeye pamoja na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel watawaomba viongozi wenzao wa Umoja wa Ulaya kuunga mkono mkataba huo.
CHANZO BBC SWAHILI