Mwanamke ajilipua kwa bomu Nigeria

Wanajeshi wa Chad wanaosaidia kupigana na Boko Haram
Mwanamke aliyejitoa mhanga alijilipuakwa bomu Jumatano katika mji wa Nigeria wa Diffa siku moja baada ya maafisa kutangaza hali ya hatari kutokana na mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Boko Haram.

Gavana wa Diffa Yakoubou Soumanou Gawo aliiambia Sauti ya Amerika kwamba mlipua mabomu huyo alikuwa amelenga kushambulia wanajeshi lakini aliishia kujiuwa mwenyewe.

Shule na biashara zilifungwa Jumatano kote katika mji huo wa Diffa na wakazi kubaki manyumbani na wengine kukimbilia usalama wao katika mji ulioko kwenye mpaka wa Niger na Nigeria.

Boko Haram walianza mashambulizi katika mji wa Diffa Ijumaa na Jumatatu, lakini wakarudishwa nyuma na wanajeshi kutoka Niger na Chad.

Vikosi vya kikanda kutoka Chad, Cameroon, Niger na Benin pamoja na Nigeria vimeahidi kuchanga wanajeshi 8,700 kupambana na Boko Haram.

Majeshi ya Nigeria yamekuwa yakipigana na kundi la Boko Haram tangu lilipoanza maasi nchini humo mwaka 2009.
CHANZO VOA SWAHILI
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company