Mwigizaji Kingwendu ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania ambao walichukua headlines za kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu 2015 ambapo wengine ni pamoja na Afande Sele, Professor Jay na Mwigizaji Frank.
Mwigizaji/Mchekeshaji Kingwendu hakufanikiwa kushinda kwenye kura za ubunge huku tiketi yake kulitaka Bunge ikiwa inapitia CUF jimboni Kisarawe mkoa wa Pwani.
Baada ya kushindwa, Kingwendu ameongea na millardayo.com na kusema yafuatayo >>> ‘Kiukweli kabisa matokeo ya mwanzo kabisa ilikua inaonyesha mimi naongoza lakini baada ya kumaliza kuhesabu kura ikaonekana amenishinda yule bwanaSuleiman Jafo wa CCM‘
‘Nimejaribu na nimethubutu kwa mara ya kwanza kugombea nafasi kubwa ya Ubunge.. nimeenda vizuri tu na sitachoka na wala sitaacha, najipanga tena kwa mara nyingine najua nimekosea wapi na ntajipanga upya na ntaenda kusomea siasa zaidi‘– Kingwendu
‘Mwaka 2020 huko nadhani nitakua niko sawa, nakwenda kusomea siasa zaidi ili niijue siasa zaidi na nijue nitamkamata wapi, kuhusu kushawishiwa kuingia kwenye siasa, hakuna mtu aliyenishawishi kugombea ubunge bali ni mimi mwenyewe niliamua baada ya kuona pia baadhi ya wasanii wenzangu wanagombania kama nilivyomuona Mr. II Sugu kipindi kile‘-Kingwendu
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago