UTATANISHI NA UKIMYA KATIKARASIMU YA KATIBA MPYA
Issa Shivji
MHADHARA WA KUAGA KIGODA CHA MWALIMU
IGODA CHA TAALUMA CHA MWALIMU NYERERKE
Copyright © Issa Shivji, 2013
Kwa dhati kabisa ningependa kuwashukuru wanakigodawenzangu, Ng’wanza Kamata, Saida-Yahya-Othman naBashiru Ally, kwa mazungumzo marefu na mabishanomakali ambayo yamenisaidia kunoa hoja zangu na kuwazayasiyowazika. Shukrani zangu kwa Walter Rodney Luanda naBashiru Ally, waliosimamia uchapishaji wa Mhadhara katikamuda mfupi wa siku mbili. Walter amekuwa bega kwa beganami kwa miaka mitano yote ya uNyagoda wangu. Amefanyakazi za Kigoda kutokana na imani na msimamo wake na siokiajira tu.Mwishowe, namshukuru sana, kwa moyo mkunjufu, SaidaYahya-Othman ambaye amehariri Mhadhara kwa ustadi wamtaalam wa lugha katika masaa ishirini na nne, tena katikasiku yake ya mapumziko maalum.
Shukrani
1. Naialika kaumu, tutafakari pamoja,Kuhusu Tunu muhimu, Rasimu ilizotaja,Kati ya Tunu adhimu, mojawapo ni umoja,Kabla ya Ukombozi, Umoja hauwi Tunu2. Umoja hauwi Tunu, Kwa taifa tegemezi,Bali umoja ni Tunu, baada ya ukombozi,Umoja hasa ni mbinu, ya kuunda mapinduzi,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.3. Uchumi wa nchi yetu, ni uchumi tegemezi,Na hasa kilimo chetu, siyo cha kimapinduzi,Na pia elimu yetu, ni chombo cha ubaguzi,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.4. Tanzania nchi yetu, sasa haina amani,Uhuru na utu wetu, kwa sasa viko rehani,Fikra na mila zetu, havina tena thamani,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu,5. Tutafakari maoni, ya waliotangulia,Ya Mkwawa na Fanoni, na ya Bibi Titi pia,Umoja walithamini, hoja waliujengea,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.6. Umoja imara hasa, siyo uliopo sasa,Huu umoja wa sasa, ni umoja wa mikasaMikasa ya kisiasa, na hila za wenye pesa,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.7. Umoja si mapatano, baina ya wala tonge,Umoja si mikutano, ya Jangwani na Kisonge,Umoja ni muungano, wa tabaka la wanyonge,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu,8. Umoja sio ubia, wa mitaji ya ‘mabwana’,Umoja ni ujamaa, wa watu wasonyonyana,Umoja kwa wenye njaa, ni nyenzo muhimu sana,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.9. Mhimili wa umoja, ni dira ya ukombozi,Na adui wa umoja, ni mifumo kandamizi,Na kitanzi cha umoja, ni sera za kibaguzi,Kabla ya ukombozi, Umoja hauwi Tunu.10. Tunataka ukombozi, wa fikra za wanyonge,Tunataka mapinduzi, ya uchumi wa wanyonge,Tunataka mageuzi, ya Umoja wa wanyongeKabla ya Ukombozi, Umoja hauwi Tunu
UMOJAHAUWI TUNU,KABLA YAUKOMBOZI
– Na Mwalimu Bashiru Ally
5
UTANGULIZI
Niliposimikwa mnamo tarehe 18 Aprili 2008 kuwa Profesa waKigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere katika Umajumui waAfrika, nilitoa mhadhara wa uzinduzi juu ya ‘Umajumui wa Afrikakatika Fikra za Mwalimu’. Sasa ninakaribia kumaliza muda wanguhapo tarehe 31 Agosti 2013, nimeona si vema nikiondoka bilakutoa mhadhara wa kuaga Kigoda, wanakigoda na wanachuowenzangu, na wale wote waliokuwa pamoja nasi katika shughulina mijadala yetu.Tumepanga mhadhara huu mapema kidogo kwa sababu mbili.Moja, wanafunzi, vijana wa Kigoda, wanaondoka leo kwendakwenye likizo yao. Ya nini kutoa mhadhara wakati wenyewehawapo? Pili, mapema mwezi ujao, pamoja na wasomi wenzangu
wawili, tumejipangia kwenda nje ya nchi kufanya utafiti wa
kuandika wasifu (biography) wa Mwalimu. Kwa hivyo, tukaonatarehe ya leo ni mwafaka.Nimegawa mhadhara huu katika sehemu kuu nne. Hoja yanguambayo itaeleza udhani (hypothesis) wangu ulioniongozakuchambua Rasimu ni sehemu ya kwanza. Sehemu ya piliitazumgumzia dhana ya ‘ukuu wa katiba’ ya shirikisho, yaani
supremacy of the federal constitution
. Kwa kirefu kidogo, ‘moyo’wa rasimu, yaani muundo na taasisi za muungano, nitazichambuakatika sehemu ya tatu. Sehemu ya mwisho, ambayo ni ya nne,kabla sijahitimisha mhadhara wangu, itakuwa juu ya matumainiya wananchi ya Tanzania Mpya.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company