Taarifa za hivi sasa kutoka nchini Tunisia zinasema kuwa kiongozi mmoja wa upinzani ameuawa.
Ripoti za vyombo vya habari nchini humo zinasema
kuwa mwanasiasa huyo Mohamed Brahmi alipigwa risasi nje ya nyumba yake
katika mji mkuu wa nchi hiyo,Tunis.Bwana Brahmi alikuwa mwanachama wa baraza la kitaifa la kikatiba, ambalo linaandika rasimu ya katiba mpya.
Mauaji yake yanakuja miezi sita baada ya kiongozi mwingine wa upinzani Chokri Belaid, kuuawa.
Mauaji ya Belaid yalisababisha maandamano makubwa na mzozo wa kisiasa, huku watu wengi wakilaumu chama tawala cha kiisilamu cha Ennahda kwa kutohakikisha kuwa ghasia za kisiasa zinasitishwa.
"Bwana Mohamed Brahmi, alipigwa risasi mbele ya familia yake , mkewe na watoto wake,Alhamisi Asubuhi.
Haijulikani nani aliyehusika na mashambulizi hayo.