Gazeti la Mawio liache upotoshaji

www.hakileo.blogspot.comNa Mwandishi Wetu
KUTOKANA na tuhuma zisizo na ushahidi zenye kulenga kushusha hadhi ya Kampuni ya Jambo Concepts (T), Ltd zilizotolewa na Gazeti la Mawio toleo la Alhamis, Aprili 22, 2013 uongozi wa kampuni hii unakanusha vikali kuhusika kwa namna yoyote na tuhuma hizo.
Pia kampuni ipo katika hatua za mwisho za kisheria kushtaki gazeti hilo na mwandishi wa habari aliyeandika habari iliyomhusisha mmoja wa wakurugenzi kuhusika katika mtandao wa dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa taarifa aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari, Dar es Salaam jana kuhusu kuchafuliwa huko, Meneja wa Kampuni ya Jambo Concepts (T) Ltd, Ramadhan Kibanike habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari “Mtandao huu hatari” ikisindikizwa na vichwa vya habari vidogo moja ikisema Ni dawa za kulevya na nyingine unahusisha vigogo kadhaa,  kwetu Jambo Concepts imelenga kuchafua mtazamo wa kampuni kwa jamii inayotuamini, pia ikiondoa hadhi ya wakurugenzi kuwa inajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.
Hii ni picha mbaya kwetu, tukikosa jibu stahiki dhamira ya gazeti hilo ambalo idadi kubwa ya waandishi wake na wanaolisimamia wanatokana na moja ya gazeti lililofungiwa na Serikali kwa muda usiojulikana ambao, mwaka juzi walipata kutaka kuandika habari ya kuichafua kampuni hii kwa taarifa za uongo.
Inashangaza sana na inatia kinyaa, kushambuliwa na watu ambao unahisi huna ugomvi nao, wakilazimisha tuhuma za kupakana matope, huku wakijua wanachokifanya si kweli na wala hakina ushahidi wake hata chembe.
Gazeti hilo limeandika “vyanzo vya taarifa vinasema, Mellisa alisindikizwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere na mmoja wa wakurugenzi wa Jambo Concepts Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Jambo Leo na Staa Spoti.
Hapa haya magazeti yanahusikaje? wakati gazeti linazungumza tuhuma? Likaendelea mkurugenzi huyo amedaiwa kuonekana na Melisa Uwanja wa Ndege Dar es Salaam,  Agosti 5.
Katika paragraph inayofuata mwandishi alimuuliza Mkurugenzi wa Jambo Concepts, akiuliza madai hayo ni kweli walifanya hivyo, lakini kinachoonekana wazi ni dhamira ya kupakana matope, kuwa wale wote walioonekana uwanja wa ndege siku hiyo walinaswa na kamera za uwanjani hapo, na Waziri Dk. Harrison Mwakyembe aliwataja wote.
Si tu kuwataja, hata aliyefika na masanduku na kuyagawanya kwa watuhumuiwa Agness Masongange na Mellisa alionekana kwenye kamera, sasa gazeti hilo linamtaja mmoja wa wakurugenzi wa Jambo kuwa alimsindikiza Melisa Agosti 5 uwanja wa ndege, sasa iweje aonekane mtu mwingine kwenye taarifa ya waziri wakati ni mkurugenzi wa Jambo? Hii inawezekana kweli? Iweje atajwe na gazeti wakati watu wote wanaohusikana na usalama wamewaona wahusika akiwemo Waziri?
Kibanike alisema tuhuma za dawa za kulevya ni zaidi ya ujambazi, ni kama ugaidi… hivi kweli unaweza ukaibuka na kumpaka matope mwenzako wakati huna uhakika na unalolisema, kama si chuki, dhamira mbaya inayokosa majibu kwetu Jambo Concept?.
Alisema kweli mwandishi huyo alijibiwa na mkurugenzi aandike kama ana uhakika kwani kwake ilikuwa habari ya kushtua, mbaya zaidi ni kuwa aliulizwa na mtu anayemfahamu.
Alisisitiza kwamba kibaya ni kusema, Mellisa aliwahi kufanyakazi City Lounge ni kweli alifanyakazi tangu kufunguliwa mgahawa huo na aliacha kazi, Februari mwaka huu, lakini je, Polisi waliokamatwa na meno ya tembo IGP naye anahusika?
Kibanike aling’aka kwamba ni upuuzi kuhusishwa kwa tukio hilo kwani si tu unamwonea, bali pia una dhamira mbaya kwake. Ukweli hakukuwa na mtu yeyote mwenye cheo cha juu ndani ya kampuni hii aliyekuwepo uwanja wa ndege siku hiyo, ushahidi wake wapi walikuwepo, utatolewa kwenye vyombo vya sheria.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company