Kulia ni mwanamama Ghislaine Dupont na wa kwanza kushoto ni Claude Verlon wanahabari wa Ufaransa waliouwawa nchini Mali siku ya Jumamosi hapa wakiwa katika majukumu yao
rt.com
Oparesheni ya kimataifa yaendelea nchini Mali kuwabaini wauaji wa waandishi wawili wa Ufaransa waliouwawa wakati wakitekeleza majukumu yao nchini humo, huku vyanzo vya polisi vikieleza kuwa tayari watu kadhaa wanashikiliwa hivi sasa.
Ghislaine Dupont aliyekuwa na miaka 57, fundi mitambo Claude Verlon mwenye miaka 55, walitekwa nyara na kisha kuuwawa makundi ya magaidi kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius kwenye mji wa Kidal siku ya Jumamosi.
Hata hivyo waziri Fabius amesema kuwa hadi sasa hakuna kundi ambalo limejulikana kuhusika na mauaji hayo na kuongeza kuwa serikali ya Ufaransa itafanya kila liwezekanalo kuwabaini na kuwaadhibu wauaji hao.
Chanzo cha polisi kutoka mjini Gao kimeeleza kuwa makumi ya watu wamekamatwa na wanashikiliwa hadi sasa kufuatia vifo vya waandisshi hao.
Hata hivyo chanzo cha karibu na waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian ambaye hakutaka kutajwa amepinga kuwepo kwa taarifa za kukamatwa na kusema kuwa wamepata taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwa wauaji.
www.hakileo.blogspot.com