Uingereza.Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amesema Tanzania inazo fursa nyingi za uwekezaji, mazingira yanayovutia, uchumi imara na sera nzuri na kuwataka Watanzania waishio nje ya nchi kutumia vipato vyao kuwekeza ili kukuza uchumi wa nchi. Akiwahutubia Watanzania waishio Uingereza katika mkutano wa kibiashara na uwekezaji, Sumaye alisema ni wazi kuwa Watanzania wanaofanya shughuli zao nje wanaingiza kipato kikubwa na kuwataka watumie kipato chao kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini.
www.hakileo.blogspot.com