Tanzania imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia tarehe 6 hadi 8
Desemba, 2013, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela.
Rais Jakaya Kikwete wa nchi
hiyo pia ameagiza kuwa katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zote
zitapepea nusu mlingoti.
Kufuatia kifo hicho Rais
Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na
kupitia kwake kwa mkewe Bi Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika
ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba,
2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
.
Rais amemuelezea Mzee Mandela
kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma
na upendo uliomwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa
moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Mandela amefariki huko
Johannesburg akiwa na umri wa miaka 95 na yeye ndiye aliyeiongoza Afrika Kusini
kutoka mikononi mwa watawala wa ubaguzi wa rangi baada ya kufungwa jela kwa
miaka 27.
Mandela alikuwa anatibiwa homa
ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.
Katika taarifa yake kwa
wananchi wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini
yuko mahali salama.
Rais Zuma amesema kuwa taifa
limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.
Mandela aliwahi kushinda tuzo
ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa
kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kutoka gerezani.
RAIS wa kwanza wa Afrika Kusini na mpinga siasa za ubaguzi wa
rangi, Nelson Mandela amefariki nchini humo akiwa na umri wa miaka 95.
Taarifa za kifo chake zimetangazwa na rais wa nchi hiyo, Jacob
Zuma ambaye amesema Mandela amefariki majira ya saa 2.50 usiku wa Alhamisi kwa
saa za Afrika Kusini.
Mandela amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwenye mapafu kwa muda
mrefu, alilazwa na baadaye kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo mauti yamemkuta
akiwa nyumbani kwake mjini Pretoria.
Tayari viongozi mbalimbali duaniani wameshaanza kutuma salamu za
rambirambi kwa familia na taifa la Afrika Kusini.
Viongozi hao ni pamoja na Rais Barack Obama wa Marekani na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon.
ARUSHA
Ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa
Arusha zimenusurika kuteketea baada ya watu wasiojulikana kuwasha moto katika
moja ya vyumba vyake jana alfajiri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema jana
kwamba walipata taarifa za kuungua kwa ofisi hizo zilizopo eneo la Ngarenaro
saa mbili asubuhi.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Aman Golugwa alisema chumba
cha kompyuta ambacho kina kumbukumbu za wanachama wote Kanda ya Kaskazini
kimeathirika.
Alisema vyumba viwili ndivyo, vimeungua kabisa na kwa bahati
nzuri moto ulishindwa kusambaa na kuzimika baada ya umeme kuzimwa.
Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Wilaya ya
Arusha, Happiness Chale ambaye aliwahi kushuhudia tukio hilo alisema, mhudumu
wa ofisi hiyo, Jenipha Mwacha alibaini moto huo baada ya kusambaa na kufika
katika maliwato
Polisi walifika mapema eneo hilo na kuweka uzio ili kuzuia watu
kuingia katika ofisi hizo pamoja na kuanza uchunguzi wa tukio hilo huku
viongozi wa Chadema Mkoa na Wilaya ya Arusha walikuwa wakitoa maelezo polisi
kuhusiana na tukio hilo.www.hakileo.blogspot.com