PICHANI NI WAJUMBE WATUME. |
NAWASALIMU KWA SALAMU ZA DEMOKRASIA,AMANI,UMOJA UPENDO NA
MSHIKAMANO; SALAMU HIZI ZIMESHEHENI HAKI,FIKRA YAKINIFU,UJASIRI,UMAKINI KAZINI,
BUSARA NA MARIFA YA HALI YA JUU.
FURAHA ILIYO IJAZA MIOYO YETU HAIPIMIKI KWA MIZANI WALA
UZANI,NA CHELEA KUIFANANISHA NA KIU ALIYO NAYO AYALA KAMA ATAMANIVYO MAJI YA
MTO,UZUNI ILIYO GUBIKA MIOYO YETU NA KUSONGA FIKRA ZETU ILIYOTOKANA NA CHANGA
MOTO MBALIMBALI ZILIZOTUSONGA IMEGEUKA NA KUWA FURAHA KUBWA.
HAKIKA HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA ,AMA KWELI BAADA YA DHIKI
NI FARAJA,RASIMU HII YA KWANZA YA KATIBA YA WANAFUNZI WA CHUO HIKI CHA A.J.T.C INAJIBU KILIO KIKUBWA NA NJAA YA MUDA MREFU
ILIYOLENGA KUJENGA MISINGI MIKUBWA YA HAKI,WAJIBU AMANI NA BUSARA MIOYONI MWETU
WANAA.J.T.C.
HII NI NJIA NJEMA INAYOASHIRIA MAFANIKIO PIA NI ISHARA YA
UKOMAVU WA KIDEMOKRASIA NA UTIMIZWAJI WA
HAKI HALI INAYO FUNGUA MIANYA YA KUKUA NA KUPENDWA KWA CHUO ZAIDI NA ZAIDI.
NDUGU WANA AJTC KWA HESHIMA NA TAADHIMA ,KWA NIABA YA TUME
YA KATIBA YA WANAFUNZI WA AJTC NINAILETA KWENU RASIMU YA KWANZA YA KATIBA
TUNAOMBA MUIPOKE E RASIMU HII YA KWANZA
KWA MIKONO YOTE MIWILI,KAMA ILIVYO ADA
RASIMU HII MTAHITAJIKA KUITOLEA MAONI .
ZOEZI HILI LA UTOAJI WA MAONI LITAFANYWA KWA MFUMO KAMALE
ULIOTUMIKA KATIKA KUKUSANYA MAONI,KATIKA HATUA HII WANAFUNZI MTAHITAJIKA
KUKOSOA AU KUICHAMBUA RASIMU HII KWA KUELEZA MAMBO AMBAYO YANGE HITAJIKA KUWEPO
NA HUENDA KWA MTAZAMO WAKO KWANAMNA MOJA AU NYINGINE HAYAKUWEKWA.
MAONI HAYO YATAPOKELEWA NA KUCHAMBULIWA NA BUNGE LA KATIBA,BUNGE
AMBALO HADI SASA TAYARI TUMEKWISHA
KUPATA WAJUMBE WAKE AMBAO WANAHUSISHA
VIONGOZI WOTE WA TUME NA WAJUMBE KUTOKA
KILA DARASA KWA KIGEZO CHA MJUMBE MMOJA KWENYE WANAFUNZI
KUMI NA TANO.
NDUGU WANAAJTC TAFADHALI KATIKA HATUA HII YA UTOAJI WA MAONI
AU MAWAZO KUHUSU VITU AMBAYO VINAHITAJIKA KUWEKWA AU KUONDOLEWA YAPASWA KUFANYIKA KATIKA GHALI YA AANI UMOJA NA UPENDO
KWANI SHABAHA YETU NI KUJENGA NYUMBA MOJA KWA HIYO HAKUNA HAJA YA KUGOMBANIA
FITO.
TUU WATOTO WA BABA MMOJA WENYE MAONO SAWA NA WENYE TOFAUTI
ZA MTAZAMO KWA HIYO KATIKA HILI SII BUSARA KUJADILI FIKRA ZA MTU WALA KUPINGA
MAONI YAKE BALI ELEZA WAZO LAKO NA MTAZAMO
WAKO BILA KUMKASHIFU WALA KIMBUGUDHI MWINGINE.
HAKIKA KAZI HII HAIKUWA RAHISI NA POPOTE PALE PENYE MAFANIKIO HAPAKOSI CHANGAMOTO, CHANGAMOTO HIZI KWA BAHATI MBAYA ZILIWAKWAMISHA BAADHI YA WAJUMBE
NA KUWAFANYA WAJIENGUWE KWENYE TUME .
KWA BAHATI MBAYA ALIYEOA TAARIFA ALIKUWA NI MMOJA TUU AMBAYE
ALIJIUZULU HUYU SII MWINGINE BALI NI NURIDINI PALLANGYO AMBAYE KUJIUZULU KWAKE
KULIKUWA NI PIGO KUBWA SIO KWA TUME TUU BALI HATA KWANGU MIMI BINAFSI KWANI NI
KIJANA MWENYE MICHANGO MIZURI NA FIKRA ANGAVU.
WAKATI TUME INATEULIWA ILIKUWA NA WAJUMBE ZAIDI YA 25 ILA WALIPUKUTIKA HADI KUFIKIA
WAJUME WASIO ZIDI 7 HALI ILIYOTULAZIMU
TUTEUWE WAJUME WENGINE ILI KUZIBA MIANYA ILIYO ACHWA WAZI.
KWA HIYO KWA HIVI SASA TUNA WAJUME 15,CHANGAMOTO HIZO NI
UHABA WA FEDHA,WAJUMBE KUTOKUWA TAYARI KUIFANYA KAZI HII PIA MATATIZO YA
KIUONGOZI NAYO PIA YALICHANGIA.
RASIMU HII INA IBARA ISHIRI NA SITA IBARA AMBAZO ZINAJENGA
UTAWALA WA HAKI NA WENYE KUWAJIBIKA,RASIMU INAKATAZA ADHABU KALI NA ZENYE
KUZALILISHA IKIWEMO KUCHAPWA FIMBO,KUPIGWA NGUMI AU MAKOFU.
PIA KUNA IBARA YA MAADILI KWA WANAFUNZI INAYO KATAZA UVAAJI
WA MAVAZI YA SIYO YA MAADILI PIA IPO IBARA YA MAADILI YA WALIMU KWA WANAFUNZI
INAYOKATAZA MAHUSIANO YA KIMAPENZI AU KUJAMIIANA BAINA YA MWALIMU NA MWANAFUNZI
ILA YALE YA UCHUMBA YANARUHUSIWA NA YAMEWEKEWA UTARATIBU MAALUMU.
KATIBA INATAMBUA HAKI ZA WANAFUNZI IKIWEMO
KUFUNDISHWA,KUPEWA ULINZI KATIKA MAZINGIRA YOTE YA CHUONI NA HOSTELI.INAKATAZA
UVUTAJI WA SIGARA BANGI NA UTUMIAJI WA MADAYA YA KULEVIA NA VILEVI KATIKA MAISHA YA HOSTELI.
PIA INATOA MIONGOZO YA KUFWATA ILI KUMTOA RAIS MADARAKANI NA
VIONGOZI WENGIME WATAKAO KIUKA MISINGI NA MAADILI YA UONGOZI.UPO UTARATIBU MWALIMU
WA MICHEZIO NA WIZARA WA NAMNAWANVYOWEZA KUTUNZA FEDHA WAZIPATAZO.
KATIKA RASIMU HII KUNA NGUZO KUU TATU,NGUZO YA KWANZA NI
BUNGE LENYE JUKUMU LA KUTUNGA SHERIA NA
KUISIMAMIA SERIKALI,NGUZO YA PILI NI SERIKALI YENYE JUKUMU LA KUWAONGOZA
WANAFUNZI NA NGUZO YA TATU NI BARAZA LA KATIBA NA SHERIA LEMYE JUKUMUSSSS LA
KUTAFSIRU SHERIA .
PIA TUME YA UCHAGUZI IPO NA KUNA IDARA MPYA YA MTHIBITI NA
MKAGUZI WA FEDHANA NA HESABU ZAKE KWA FEDHA ZA WANAFUNZI KWENYE NGUZO ZOTE.
MUNGU IBARIKI RASIMU HII,MUNGU IBARIKI A.J.T.C
ASANTE KWA KUNISIKILIZA.