Kiongozi wa chama cha upinzani nchini India, Hindu nationalist, Narendra Modi (katikati), akifurahia na wafuasi wake ushindi wa chama chake kabla zoezi la kuhesabu kura halichamalizika.
REUTERS/Amit Dave
Na
RFIChama cha upinzani kinachoongozwa na Narendra Modi kina imani kama kitashinda uchaguzi mkuu uliyomalizika jana,baada ya kura za mwanzo ziliyohesabiliwa kuonyesha kuwa chama hicho kinaongoza kwa sehemu kubwa.
Magazeti nchini India leo hii yameandika wamba kiongozi wa upinzani Narendra Modi, akaribia Ikulu, huku mengine kama Hindustan Times likiandika Karibu Modi.
Utabiri wa kura hizi za maoni huwa zinatimia hasa katika nchi kubwa zenye wapiga kura wengi kama India ambayo zaidi ya wapiga kura milioni 800 walipiga kura kwa zaidi ya mwezi mmoja na kumaliza jana Jumatatu.
Kama inavyotabiriwa ikiwa chama cha upinzani cha Bharatiya Janata Party kitashinda, kitakiondoa chama tawala cha Congress party ambacho kimekuwa uongozini kwa miaka 10 sasa.
Kituo cha kupigia kura kaskazini mashariki mwa India, aprili 7 mwaka 2014.REUTERS/Adnan Abidi
Wakati matokeo ya mwisho yakisubiriwa siku ya Ijumaa baadhi ya wachmabuzi wa siasa nchini India wametoa wito kwa wafuasi wa chama cha upinzani kuacha sherehe za mapema kwani chochote kinaweza kufanyika na matokeo kubadilika.
Upinzani unasema kuwa una uhakika wa kushinda viti vya ubunge 300 kati ya 543 vinavyowaniwa na hivyo kuunda serikali ijayo.