Jenerali wa Sudan Kusini auwawa Bor.


Mmoja wa wanajeshi wa jeshi la Sudan Kusini.
Mapigano makali yamezuka nje ya mji mkuu wa Sudan Kusini wa Bor na Jenerali mmoja wa jeshi la Sudan Kusini ameuwawa.
Mwandishi wa BBC anasema vikosi vya serikali vinazidi kuelekea karibu na mji wa Bor ambapo kumekuwa na mapigano ya kutegeana baina ya majeshi ya serikali na vikosi vya waasi vinavyomtii aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.

Mwandishi wetu amesema pia ameshuhudia miili ya watu ikiwa chini na vifaru vikiwa vimelipuliwa vibaya pembezoni mwa barabara.

Pande pinzani nchini humo zinataraji kuanza mazungumzo ya ana kwa ana mjini Adis Ababa kujaribu kumaliza wiki tatu za mapigano.

Kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Sudan kusini Nial Deng Nial amesema kuwa ni muhimu kwamba viongozi kuzungumzia kuhusu kusitishwa kwa vita.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company