Mh. Rais Kikwete Aalikwa Nigeria na Rais Jonathan

Rais wa Nigeria Mheshimiwa Goodluck
Jonathan amemwalika Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa
Taasisi ya Uchumi Duniani Afrika (WEF-Africa)
unaofanyika katika mji mkuu wa Nigeria wa
Abuja mwezi Mei mwaka huu.
Rais Jonathan ametoa mwaliko huo kwa Rais
Kikwete wakati viongozi hao wawili
walipokutana na kufanya mazungumzo leo,
Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya
Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako
viongozi hao wanahudhuria wa Mkutano wa
Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –
WEF.
Rais Kikwete amekubali mwaliko huo wa
kuhudhuria Mkutano huo uliopangwa
kufanyika Mei 7-9 mwaka huu mjini Abuja,
Nigeria.
Mkutano huo kati ya viongozi hao wawili
umehudhuriwa na Mawaziri wa Nigeria wa
Mambo ya Nje na Fedha na Uchumi.
Nigeria inakuwa nchi ya nne katika Afrika
kuandaa mkutano huo.
Kwa miaka mingi, mkutano huo wa WEF-
Africa ulikuwa unafanyika Cape Town, Afrika
Kusini mpaka Tanzania ilipofanikiwa kuwa nchi
ya kwanza ya Afrika nje ya Afrika Kusini
kuandaa Mkutano huo mwaka 2010.
Tokea wakati huo, Ethiopia imeandaa
mkutano huo na sasa Nigeria.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
23 Januari, 2014


Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company